Mourinho na Wenger Wapinga Goli la Ugenini, UEFA Wakubali Kulitoa

Mourinho na Wenger wapinga goli la ugenini, UEFA wakubali kulitoa
Makocha wa timu kubwa barani Ulaya wamekitaka chama cha mpira barani humo (Uefa) kufanya mabadiliko ya kanuni ya faida ya magoli ya ugenini katika michuano ya Ulaya.Naibu katibu mkuu wa Uefa Bw Giorgio Marchetti amesema chombo hicho kitafanya marekebishi ya kanuni ya faida ya goli la ugenini.

Makocha hao pia wamependekeza msimu wa usajili uhitimishwe kwa wakati mmoja katika ligi zote kubwa za Ulaya.

“Makocha wanasema kufunga magoli katika viwanja vya ugenini si tena jambo gumu kama ilivyokuwa huko nyuma,” amesema naibu katibu mkuu wa Uefa Bw Giorgio Marchetti.  “Wanataka kanuni hiyo ifanyiwe maboresho na hicho ndicho tutakachokifanya.”

Mkutano huo wa mwaka umehudhuriwa na makocha wa Manchester United Jose Mourinho, Unai Emery wa Arsenal pamoja na mtanguilizi wake Arsene Wenger, Massimiliano Allegri wa Juventus, Julen Lopetegui wa Real Madrid, Carlo Ancelotti wa Napoli na Thomas Tuchel wa Paris St-Germain.

Kanuni ya faida ya goli la ugenini ilianzishwa mwaka 1965 kama mbadala wa kurusha sarafu ama kuandaa mechi ya marudiano katika uwanja huru (usio wa timu yeyeote shindani) pale ambapo matokeo ya mechi mbili za timu zinazoshindana yanapokuwa sare. Kitambo hicho hali ya usafiri kutoka nchi moja kwenda nyengine ilikuwa sio rahisi kama zama za sasa.

Pale matokeo yanapokuwa sare, timu ambayo ilifunga magoli mengi ilipokuwa ugenini huibuka na ushindi. Kanuni hiyo bado inatumika mpaka sasamiaka 53 toka ilipoanzishwa.

Bw Marchetti pia amesema makocha hao wanaamini kanuni hiyo imekuwa ikileta matokeo kinyume na yale ambayo yalikusudiwa. Pamoja na kuwa chachu kwa timu iliyougenini kushambulia sana pia inaifanya timu ya nyumbani kujilinda sana ili kuepusha kufungwa goli ambalo linaweza kuwaletea madhara makubwa ya kung’olewa mashindanoni.



Kuhusu dirisha la usajili, amesema makocha wametaka mfano wa England na Italia ufuatwe nan chi nyengine ambapo usajili hufungwa kabla ya ligi zao kuanza.

Nchini Uhispania na Ujerumani dirisha la usajili husalia wazi mpaka mwisho wa mwezi wa Agosti.



“Makocha wanataka kuwe na mfumo mmoja wa dirisha la usajili ambalo litafungwa bara zima kabla ya ligi hazijaanza. Lengo hapa ni kuwawezesha wote wawe katika mstari mmoja mnyoofu,” amesema Marchetti.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad