Gari lililokuwa limebeba waandishi wa habari wa Mkoa wa Simiyu limepata ajali kwenye msafara wa Rais John Magufuli wilayani Meatu ambapo liligongwa na magari mengine kwa nyuma.
Waandishi wa habari watatu, Adan Mhando wa Channel Ten, Faustine Fabian wa Mwananchi, Rehema Evansi wa Azam TV, na Mpiga picha wa ITV, wamepata majeraha madogomadogo na wamekimbizwa hospitali ya wilaya Meatu.
Wengine waliokuwemo katika ajali hiyo na kunusurika ni Berensi China,Samwel Mwanga,Derick Milton,Costantine Mathias na Rehema Evance.
Poleni ndugu kwa ajali na pia binafsi namshukuru sana Bwana Mungu aliyewanusuru
ReplyDeleteBw Kigwangala anaendeleaje, mbona hakuna update on his progress, wanaomuombea wangefurahi kujuzwa
ReplyDelete