Aliyekua Msaidizi wa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Freeman Mbowe amesema hakuna kiasi chochote alichopewa na CCM ili ajiunge nayo huku akisema utendaji kazi wa Rais John Magufuli ndio uliomshawishi kujiunga na chama tawala.
Bernad Mwakyembe amefichua kuwa wapo makada na wabunge wa Chadema waliondoka kwa sababu za kutoelewana na viongozi wakuu akiweno Mwita Waitara mbunge wa Ukonga.
Amesema kuna sababu nyingi zilizomfanya ajiunge na CCM ambapo nyingi ni kutokana na Rais Magufuli kutekeleza sera ambazo Chadema ilizinadi mwaka 2015 katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.
Mwakyembe ambaye pia alikua ni Makamu Mwenyekiti wa Chadema Dar es Salaa amesema Rais Magufuli amefanya mambo makubwa kwa muda mfupi ikiwemo ujenzi wa viwanda nchi nzima, daraja la Mfugale lililopo Tazara pamoja na bwawa kubwa la ufuaji umeme Stigler Gorge.
" Rais anafanya kazi kubwa tangu aingie madarakani, amesimamia kwa nguvu suala la watumish hewa na watu zaidi ya 12,000 ambao walikua na vyeti feki hivyo kuokoa kiasi kikubwa cha fedha," amesema Mwakyembe.
Amesema Rais Magufuli amepunguza matumizi makubwa ya serikali jambo ambalo limesaidia Serikali kuweza kujitegemea na hivyo kuweza kufanya mambo makubwa ikiwemo ununuzi wa ndege ambazo amesema licha ya Chadema kupinga bado wanaongoza kuzipanda.