Mtanzania aishangaza Dunia, amchapa bondia wa Uingereza


BONDIA raia wa Tanzania, Hassan Mwakinyo amemchakaza bondia, Sam Eggington raia wa Uingereza kwa KO katika raundi ya pili mjini Birmingham nchini Uingereza. 

Pambano hilo lililofanyika usiku wa jana, lilishuhudia Mwakinyo akiendeleza rekodi nzuri katika michezo yake huku akionekana kumshinda mpinzani wake tangu mwanzo wa mchezo kwenye pambano lililochukua takribani dakika 10 kupata mshindi. 

Hassan Mwakinyo (23) ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBA sasa ameshinda michezo 12 kati ya 14 aliyocheza huku akipoteza mapambano mawili pekee. 

Mpinzani wake, Sam Eggington ambaye ni bingwa wa mkanda wa WBC sasa anakuwa amefikisha mapambano 28 aliyopigana, akishinda 23 na kupoteza mapambano matano ukiwemo huo wa jana dhidi ya Mwakinyo. 

Kipigo hicho cha Eggington kinampunguzia nafasi nzuri ya mipango yake ya kuandaa mapambano makubwa mwaka huu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad