Mungu Atanipa Mume Wa Kunioa- Hamisa Mobetto

MWANAMITINDO ambaye ni mzazi mwenza wa mwanamuziki mwenye jina kubwa ndani na nje ya nchi, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Hamisa Mobetto ameliambia Ijumaa Wikienda kuwa, mwanaume atakayekuwa mumewe wa ndoa anayempangia ni Mungu na siyo watu mitandaoni.



Hamisa alisema yeye ni mwanamke na kamwe hawezi kupinga kuwa atakuja kuwa mke wa mtu, lakini yote hayo yanapangwa na Mwenyezi Mungu na siyo dua za binadamu.



“Watu wanashindwa kuelewa kwamba hakuna kitu sisi wanadamu tunajipangia bali muumba wetu, kwa hiyo hata mimi mume wangu atakayenioa anapangwa na yeye maana wenye kutabiri ni wengi na siyo kwamba ukizaa na mtu ndiyo lazima akuoe yeye,” alisema Mobetto.



Hamisa amekumbana na changamoto nyingi za kubezwa na kutukanwa kwenye mitandao ya kijamii baada ya kuzaa na Diamond ikionekana yeye ndiye chanzo cha mwanamuziki huyo kuachana na mzazi mwenzake, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad