Museveni Atoa Amri Kusitisha Posho na Marupurupu

Museveni Atoa Amri Kusitisha Posho na Marupurupu
Rais Yoweri Museveni ametoa amri ya kusitishwa mara moja nyongeza ya posho na marupurupu mengine kwa watumishi wa umma, nyongeza ambazo ziliidhinishwa Juni 2018.


Baraza la Mawaziri lilikuwa limepitia na kuidhinisha viwango hivyo kwa watumishi wa umma kwa sababu vile vya awali vilikuwa vidogo sana ikilinganishwa na ughali wa maisha.

Hata hivyo, uamuzi huo haukumridhisha Museveni ambaye katika barua yake ya Agosti 30, 2018 alimwagiza Waziri Mkuu Dkt. Ruhakana Rugunda kuitisha kikao cha Baraza la Mawaziri mapema mwezi huu, kubatilisha uamuzi wa awali.

"Nimearifiwa kwamba Wizara ya Utumishi imeongeza posho kwa kiwango kikubwa, hali ambayo ilijadiliwa na Baraza la Mawaziri baada ya kukamilika mchakato wa uandaajiwa bajeti. Fedha zinazohitajika kutekeleza nyongeza hizi haikuwa imejumuishwa katika bajeti iliyopitishwa, kwa nini Baraza la Mawaziri liliidhinisha posho mpya wakati bajeti kuu ilikuwa imepitishwa?”, ilihoji sehemu ya barua ya Museveni.

Katika nyongeza hiyo mpya, baadhi ya wanufaika wakubwa ni makamu wa rais ambaye posho yake kwa safari za ndani iliongezwa kutoka Shilingi 210, 000 hadi 500, 000 na waziri mkuu aliongezewa posho kutoka Shilingi 200,000 hadi Sh 490,000.

Huku wanufaika wengine ni naibu waziri mkuu aliyepandishiwa kutoka Shilingi 195,000 hadi 480,000, wakati posho za mawaziri zilipanda kutoka Shilingi 190,000 hadi 475,000 na manaibu wao kutoka Shilingi 185,000 hadi  470,000.

Rais Museveni alihoji kwa nini Baraza la Mawaziri liliidhinisha nyongeza siku kadhaa baada ya bajeti ya serikali kuidhinishwa ilhali wanajua hakukuwa na fedha za ziada kugharimia aina hiyo ya matumizi katika Bajeti ya 2018/19.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad