Mv Nyerere Imezama kwa Mipango ya Mungu Ila Wengi Wamekufa kwa Mipango Yetu- Idriss

Mv Nyerere Imezama kwa Mipango ya Mungu Ila Wengi Wamekufa kwa Mipango Yetu- Idriss
Mchekeshaji Idris Sultan ameamua kutoa ya moyoni kuhusiana na ajali ya Mv Nyerere iliyotokea siku ya jana huko Jijini Mwanza na kusababisha vifo vya watu zaidi ya 80 hadi kufikia leo.

Kupitia ukrasa wake wa twitter idris aliandika ujumbe mzito ambao ulikua na maana kubwa na kusema hivi

Nieleweke vyovyote mtakavyoniamua ila Mv Nyerere imezama kwa mipango ya mungu ila wengi wamekufa kwa mipango yetu


Ajari ya Mv nyerere ilitokea jana mchana huku chanzo kamili cha ajali hiyo akijatolewa rasmi ila kwa taarifa za awali zinadai kuwa kivuko hicho kilibeba abiria wengi ambao inasemekana ni watu 400 na kilikuwa kinakaribia kutia nanga na kubaki umbali wa mita mia mbili hivyo idadi kubwa ya watu walikuwa wanasogea mbele ili kuwahi kushuka ndipo kivuko hicho kikazidiwa upande mmoja na kupinduka.

Post a Comment

2 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.
  1. sasa si ungekuwa mstari wa mbele n wewe kwenda kuokoa hata uonkoaji unamtegemea mungu sio rahisi kama unavyofikiria hata waokoaji wenyewe wako hatarini ni kuwaombea tu ,mtu uko dar si ajabu hata ziwa hulijui usicheze na maji kaka.

    ReplyDelete
  2. MUNGU HAPANGI MAMBO KAMA HAYO NI MIPANGO YA SHETANI NA WANADAMU

    ReplyDelete

Top Post Ad

Below Post Ad