MV Nyerere: Mtaalamu wa Kuhifadhi Maiti Asimulia Zoezi Lote Lilivyokuwa

MV Nyerere: Mtaalamu wa Kuhifadhi Maiti Asimulia Zoezi Lote Lilivyokuwa
MTAALAM wa kuhifadhi maiti katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure, David Maliganya, ameelezea ni kwa jinsi gani alivyofanikisha zoezi la kuhifadhi miili ya watu waliofariki katika ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere katika Ziwa Victoria mkoani humo.



Maliganya ambaye alisafirishwa kutoka Jiji la Mwanza hadi wilayani Ukerewe kwa ajili ya zoezi hilo, amesema amefanya kazi hiyo kwa miaka 12 na ameshazoea changamoto za kuhifadhi maiti zitokanazo na ajali za majini.



“Miili inayotokana na ajali za maji  huibuka siku mbili au tatu ikiwa imeharibika vibaya, imevimba kwa sababu ya kupingana na ile hali hiyo ya kifo, hivyo inahitaji ujuzi mkubwa kuihifadhi kwa ajili ya kusafirishwa na maziko.



“Wana-Ukerwe walivyoniona mioyo yao ilitulia kwa sababu wananifahamu, nimeshawahi kufanya hapa kazi, walifahamu kabisa miili ya ndugu zao wataipata ikiwa imeandaliwa vizuri. Wakati naanza kufanya kazi hapa Ukerewe wengine waliniita mchawi, waliamini mambo ya kishirikina, na watu walikuwa hawataki kugusa maiti za ajali ama za kuvimba matumbo.



“Wapo ambao wanaamini ushirikina kwamba wakichukua kamba ya mtu aliyejinyonga eti watapata samaki wengi ziwani, wengine wanaamini ushirikina wa maji ya kuoshea maiti.  Ningekuwa na tamaa ningekubali wakanipa pesa na ningekuwa tajiri sana lakini siamini hivyo vitu; nafanya kazi yangu kwa weledi kama nilivyosomea,” alisema Maliganya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad