Mwanafunzi wa Chuo Cha Mipango Mbaroni Kwa Ujambazi


James Senya(21) anashikiliwa kwa tuhuma za kujihusisha na makosa ya uvunjaji na wizi katika maeneo mbalimbali jijini Dodoma

Kamanda wa Polisi, Gilles Muroto amesema wamemkamata baada ya kufanyika doria na kugundua kuwa anashirikiana na wahalifu wengine kufanya vitendo hivyo

Mwanafunzi huyo wa mwaka wa kwanza amekuwa akiwachorea wahalifu ramani ya kuvunja na kupora mali katika nyumba za watu

Aidha, amekamatwa na watu wengine watano anaodaiwa kushirikiana nao ambao ni Ayubu Hosea(23), Saudi Mosse(23), Semen Njaid(24), Salum Abdallah(16) na Godfrey Mashauri (26)

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad