Polisi nchini Kenya imemkamata Gavana Okoth Obado wa jimbo la migori magharibi mwa nchi hiyo.
Obado ataaendelea kuzuiliwa huku uchunguzi kuhusiana na kifo cha mwanafunzi wa chuo kikuu, Sharon Otieno ukiendelea.
Maafisa kutoka kitengo cha upelelezi wa uhalifu wa jinai, DCI wamemhoji kwa saa kadhaa leo.
Obado amekanusha madai ya kuhusika na mauaji ya mwanafunzi huyo ambaye inasadikiwa alikuwa mpenzi wake.
Polisi inasema Gavana huyo wa jimbo la Migori magharibi mwa Kenya atafikishwa mahakamani mjini Nairobi siku ya Juma tatu.
Wiki iliyopita, Obado aliwaambia polisi mjini Kisumu kwamba yeye binafsi angelipenda kuwajua wauaji wa Sharon ni kina nani.
Wakili wake Obado, Cliff Ombeta anasema mteja wake hana hatia na kwamba amewaeleza polisi kila kitu alichofahamu kuhusiana na kesi hiyo.
Kupatikana kwa mwili wa Sharon
Mwili wa Sharon ulipatikana ukiwa umetupwa kichakani eneo la Oyugis, Homa Bay mnamo 5 Septemba.
Kuuawa kwa kudungwa visu
Mtaalamu mkuu wa upasuaji wa maiti Kenya Johansen Oduor, baada ya kuuchunguza mwili wa marehemu, alisema mwanamke huyo huenda alifariki kutokana na kuvuja damu sana.
Alikuwa amedungwa kisu mara nane.
Mwili huo pia ulikuwa na alama za kukabwa shingoni, na alama nyingine zinazoashiria kwamba alijaribu kujiokoa.
Mwanasiasa Mkuu Kenya Kenya Akamatwa na Polisi kwa Mauaji ya Mwanafunzi
0
September 22, 2018
Tags