Mzee Akilimali Ampa Somo Kali Haji Manara

Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, amemtaka Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kupunguza maneno Baada ya kushindwa kutamba mbele ya Ndanda FC Jana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kwa kutoka nayo suluhu ya kutofungana.

Mzee Akilimali ameibuka na kumpa pole Manara akisema kuwa ni mdogo wake na hawezi sana kumtania japo amemuomba kupunguza zaidi maneno kuliko vitendo.

Mzee huyo kwa busara kabisa amemtaka Manara kupunguza zaidi tambo za kujigamba na badala yake amemuelewesha kuwa kwenye mchezo huwa kuna matokeo matatu.

Katibu huyo wa Baraza la Wazee ameeleza kuwa Manara amekuwa akiwatania zaidi Yanga huku akiipa sifa kubwa Simba na kusahau kama mpira huwa na matokeo ya aina yake.

Mzee huyo anaamini suluhu waliyoipata Simba dhidi ya Ndanda itakuwa imewapa funzo kuwa hii ndiyo na kila mechi inakuwa na changamoto zake.

"Unajua huyu mdogo wangu nadhani bado hajaitambua ligi vizuri, namshauri tu vizuri kwa maana siwezi kumtania ni vema akaelewa kuwa mchezo una matokeo matatu. Namuomba apunguze zaidi tambo kwa timu yake na atambue kuwa si kila mechi unaweza kushinda" alisema.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad