Mzungu Simba Awataka Mabeki Kuwa Makini na Makambo

Mzungu Simba  Awataka Mabeki Kuwa Makini na Makambo
Mzungu wa Simba, Adel Zrane raia wa Tunisia, anafahamu uwezo wa mshambuliaji wa Yanga, Heritier Makambo, hivyo amewaonya mabeki wa Simba kwa kuwataka wawe makini naye.

Simba na Yanga zinatarajiwa kucheza kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar ukiwa ni mchezo wa kwanza wa ligi kuu baina ya timu hizo.

Zrane ambaye ni kocha wa viungo wa Simba, alionekana akiwasisitiza mabeki namna ya kumdhibiti Makambo katika mazoezi yaliyofanyika juzi Alhamisi kwenye Uwanja wa Boko Veterani.

“Makambo kama mshambuliaji ana wajibu wa kuisaidia Yanga na ni majukumu yake pia, kwa kiwango chake bora kabisa anaweza kuitishia beki ya Simba, hivyo ni lazima kwa mabeki kuchukua tahadhari kwa mchezaji huyu,” alisikika Zrane akiwaambia wachezaji wake.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad