Nai Atangaza Vita na Wasanii wa Bongo Awapa Siku Saba

Nai Atangaza Vita na Wasanii wa Bongo Awapa Siku Saba
Video vixen' maarufu na 'Makeup Artist' ambaye pia ni mpenzi wa rapa Moni Centrozone, Nai, amewapa siku saba mastaa wa bongo fleva kulipa fedha wanazodaiwa na mrembo huyo za 'makeup' na wakishindwa kufanya hivyo adai atawaanika hadharani.


Nai amebainisha hayo alipokuwa anazungumza kwenye kipindi cha eNewz inayorushwa na tinga namba moja kwa vijana EATV, na kusema kuwa kuna baadhi ya wasanii watatu amekusudia kuwadhalilisha mitandaoni endapo hawamtalipa pesa yake kwa kuwa anawaona wamekusudia kumuharibia biashara yake.

"Ninawapa siku saba ninao wadai wanilipe fedha zangu na wasionilipa wakae watambue watakutana na deni lao eNewz, yaani nitamuanika kuanzia juu hadi chini. Katika hao mastaa watatu ninao wadai kuna mmoja alinipa pesa nusu za ku-shoot video lakini hadi leo hajanimalizia pesa ninayodai", amesema Nai.

Pamoja na hayo, Nai ameendelea kwa kusema kuwa "kiukweli nipo serious kwasababu mimi sipendi kumsumbua mtu kila muda kumpigia simu kudai fedha, 'so' naona kama wanataka kunirudisha nyuma".

Kwa upande mwingine, Nai amedai kwa sasa ameingiwa na uoga wa kufanya kazi na msanii ambaye hana fedha kamili ya kufanyiwa kazi yake maana anahofia wasije wakaacha kumlipa na kumrudisha nyuma katika utendaji wa kazi yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad