Namtamani Fid Q na Joh Makini - Wakazi


Rapa Wakazi amefunguka na kudai anatamani kufanya 'collabo' na mkongwe Fid Q pamoja Joh Makini ili kusudi kuweza kuupandisha hadhi zaidi muziki wa hiphop kiujumla.


Wakazi ameeleza hayo akiongea na eNewz na kusema endapo itaweza kutokea 'collabo' hiyo, pia itasaidia kufuta dhana potofu iliyojengeka vichwani mwa watu kuwa kuna hiphop ngumu na ile rahisi na kusahau kwamba muziki wa hiphop unazungumzia maisha.

"Natamani sana kuona collabo baina yangu na Fid Q pamoja na Joh Makini naamini tutaweza kubadilisha upepo na mtazamo wa hiphop. .....Kwa wasanii ambao wamelishwa dhana ya kwamba kuna hiphop ngumu na rahisi waendelee kuamini hivyo au waachane na hiyo dhana warudi kwenye mstari ili tuweze kupeleka muziki wa hiphop mbali. Mimi naimba hiyo hiphop wanayosema ni ngumu na nina mashabiki wengi wa kike tena wazuri kuliko hata hao wanaoimba hiyo hiphop rahisi", amesema Wakazi.

Aidha, Wakazi amesema hiphop ni mtazamo wa mtu katika kufikiria juu ya jambo fulani hivyo endapo mtu ataona hajauelewa muziki wa hiphop fulani basi atambue kuwa hayupo katika uhalisia uliyozungumziwa ndani ya wimbo huo husika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad