Nassari Ajitofautisha na Lema, Msigwa na Heche


Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki Joshua Nassari amesema yeye sio mbunge wa mitandao ya kijamii na kudai kazi yake ni kuwatumikia wananchi wa jimbo lake ambae ndio walimchagua.


Pichani kutoka kulia ni Mbunge wa Arumeru Mashariki (CHADEMA) Joshua Nassari, katikati ni Godbless Lema mbunge wa Arusha mjini (CHADEMA) na Mchungaji Peter Msigwa mbunge wa Iringa mjini (CHADEMA).

Akizungumza na www.eatv.tv iliyotaka kufahamu juu ya ukimya wake hali inayoonekana kuwa tofauti na baadhi ya wabunge wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Joshua Nassari amesema haumizwi kichwa na baadhi ya watu wanaodai yuko kimya.

www.eatv.tv; “Mheshimiwa Nassari habari, watu wanauliza mbona upo kimya sana hasa kwenye mitandao ya kijamii tofauti na wabunge wenzako kama wakina Godbless Lema, Peter Msigwa na John Heche.?

Joshua Nassari; Naomba nipigie baada ya dakika 3. Ila kwa hao wanaodai niko kimya wakina nani,?  kama ni watu wa mtandaoni mimi sio mbunge wa mtandao ni mbunge wa Arumeru ninawatumikia wao.

Kisha akakata simu na hakupokea hata alivyopigiwa kwa mara nyingine.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad