"Ndio kwanza Nimeanza..Mtanikoma"- Hamisa Mobetto


Baada ya kuachia video ya wimbo wake mpya wa 'Madam Hero', iliyoshika namba moja katika mtandao wa 'Youtube' kwa Tanzania, mwanamitindo maarufu na mbunifu wa mavazi nchini Hamisa Mobetto, amesema ataendelea kujikita katika tasnia hiyo ya uimbaji ambayo inampa mafanikio makubwa kwa sasa.


Akizungumza na www.eatv.tv, Mobetto amesema hakutegemea kupata mapokezi anayopatiwa ndani ya tasnia hiyo ,hususani kwa mashabiki na Wadau wakubwa wa muziki nchini uku akidai kuwa muziki hauto mzuia kufanya shughuli zake za awali ikiwemo mitindo, ubunifu na uigizaji

“Sikutegemea kama itapokelewa vizuri hivyo,kwani wimbo huu nilirekodi muda mrefu tangia mwaka jana, na sikuwa na huwakika kama nitaitoa, kwani sikufahamu kama mashabiki watanielewa lakini nimefurahi na nina mshukuru mungu umekubalika”._

Kwa upande wa bifu kati yake na msanii Ray C, ambapo awali mwanadada huyo alimkashifu Mobetto na wimbo huo mpya kupitia instagram, Mobetto amesema.

“Unajua huyo dada sijawahi kumuona live yaani, na mwanzoni sikujua kama ananiongelea mimi na sikuwahi kumjibu chochote kuhusiana na hilo,na binafsi napenda mziki wake na wengi tumekua tukimsikiliza, kama ameposti video yangu nashukuru.Unajua nchi za wenzetu wakifanya mabifu wanatengeneza pesa ila sisi kwetu haina faida”.

Kuhusiana na suala la kuitwa Tanzania Sweetheart, Mobetto amesema kwa sasa hataki kuhusishwa na mambo hayo hususani muigizaji wa filamu nchini Wema Sepetu ambaye amekiri kutokuwa na mahusiano nae mazuri kwa sasa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad