Ndoa Haina Kipaumbele Kwenye Maisha Yangu- Wolper

Ndoa Haina Kipaumbele Kwenye Maisha Yangu- Wolper
Mbunifu wa mavazi na Muigizaji wa Bongo movie Jacqueline Wolper ameibuka na kuweka wazi kuwa suala la ndoa halina kipaumbele sana Kwenye maisha yake.

Wolper ameshawahi kulalamika sana kuhusu suala la kuumizwa na mapenzi na kudai kila mwanaume ambaye ameshawahi kuwa naye Kwenye Mahusiano ameishia kumuumiza na kumtenda:

Kwenye Interview aliyofanya hivi karibuni, Wolper amefunguka kuwa akiwa Kwenye Mahusiano kwa sasa ndoa haina kipaumbele kwani ameshatendwa sana kimapenzi:

Kwenye mapenzi silipi sana suala la kuolewa kipaumbele kwa kuwa nimeshawahi kuumizwa sana kimapenzi, lakini namuomba huyu nitakayempata nitaanza kulifikiria hilo suala maana nataka nimpende kuliko mwanaume yoyote yule ambaye nimewahi kuwa naye”.

Wolper amewahi kukiri kuwa Harmonize ni moja kati ya wanaume ambaye amewahi kumuumiza sana kwani alimuacha na kuamua kuwa na mwanamke mwingine kwa ajili ya pesa wakati yeye alimuacha mwanaume wake ambaye alikuwa na pesa sana kwa ajili yake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad