Ni kweli Samatta Kaombwa na Genk Avae Jezi Namba 10 na Aiache 77?

Mashabiki wa soka ninayo exclusive interview na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ambaye anaichezea club ya soka ya KRC Genk ya Ubelgiji Mbwana Samatta ambaye amefunguka kuhusiana na ishu yake ya kubadilisha namba ya jezi kutoka namba 77 hadi 10.

Mwanzo zilisikika tetesi kuwa Mbwana Samatta baada ya kufika KRC Genk alikuwa akitumia jezi namba 77 lakini baadae akaanza kutumia jezi namba 10 ambayo hata timu ya taifa ndio anaitumia kwa sasa.

Stori zikawa zinasema baada ya viongozi wa Genk kuona uwezo wa Samatta wakamuomba atumie jezi namba 10 ambayo inaaminika mara nyingi inavaliwa na wachezaji ambao wanafanya vizuri au ni mastaa katika club husika, Samatta katika exclusive interview na kuomba ufafanuzi kuhusiana na taarifa hizo.

“Nadhani sio jambo lenye ukweli sana au kubwa kiasi hicho kwa sababu kwa wenzetu Ulaya, nafikiri jezi ina maana sana kwa mchezaji aliyekuwa kafanya mambo makubwa sana katika klabu na kwa Genk hakukuwa na mtu ambaye alikuwa amefanya vitu vikubwa zaidi na alikuwa anatumia jezi namba 10 hivyo mimi niliipata kawaida”
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad