Nikki wa Pili Autamani Upinzani ..Ashangaa Viongozi Kukimbia Majimbo yao


Msanii kutoka kampuni ya Weusi, Nikki wa Pili amesema ana huzunika kuona hali ya ushindani wa kisiasa nchini kupungua kutokana na baadhi ya viongozi kukimbia majimbo yao na kwenda chama kingine kwa madai kitendo hicho kinaweza kuwafanya wabweteka kwa kuwa wanajua hakuna wakushinda nao.


Nikki wa Pili ameeleza hayo alipokuwa anapiga stori na www.eatv.tv na kusema kuwa anatamani hali ya kisiasa ya mwaka 2015 ilirejea katika miaka hii, ili siasa ipate kuchangamka na kuwapa fursa wananchi katika kutatuliwa matatizo yao kwa haraka.

"Nina huzunika kuona ambavyo upinzani unapungua nchini kwenye masuala ya kisiasa, kwasababu ushindani ukipungua hakuna wa kumpinga mwenzake. Pia kwa demokrasia ya vyama vingi sio jambo jema hilo, mimi napenda kuona vyama vyote vikiwa na nguvu ili viweze kuchuana pamoja na kuweza kutatua kero za wananchi", amesema Nikki wa Pili.

Pamoja na hayo, Nikki wa Pili ameendelea kwa kusema kuwa "chaguzi zilizopita zilikuwa na ushindani mkali, lakini sasa hivi tunaona baadhi ya viongozi wakihama kutoka upande mmoja na kwenda kwengine".

Kauli hiyo ya Nikki wa Pili imekuja baada ya kuwepo matukio mengi ya kisiasa yakihusisha wanachama wake kuhama na kwenda sehemu nyingine kutokana na sababu mbalimbali ambazo wao wameziona kwa upande wao ni kero wakiendelea kuwepo sehemu hiyo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad