Nisha Awatolea Povu Zito Wanaomsema Anasura Mbaya

Msanii wa filamu Bongo, Nisha amewatolea povu zito  wale wanaokuwa wakikosoa muonekano wake.

Muingizaji huyo amesema kuwa kujisifia una muonekano mzuri wakati hauna bahati haina maana yoyote.

==>>Kupitia ukurasa wake wa Instagram ameandika;

"Halafu nyie mnaosema nina shepu mbaya hivi mshawahi kuhongwa hata Mil. 5 cash nyie? maana msije kujisifu shepu nzuri bahati 0. Nguvu yenu ya vocha achilia masuala ya kuzisaka wenyewe huko ndo usithubutu,wanawake wabaya tunajua kuzisaka chapaa hatari.

"Uzuri wangu kama bungo uko ndani kwa ndani babu weee ukiona picha lazma mate yakutoke na uzuri akili,tabia na mipango ndo maana NAJIKUBALI. 📸 @mubast." Ameeleza Nisha.

Licha ya kufanya vizuri katika filamu, pia Nisha ameingia kwenye muziki wa Bongo Fleva ambapo hadi sasa ametoa nyimbo mbili, Bachela na Yeye.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad