''Nitaanza Kwenda Ofisini na Baiskeli'' - Paul Makonda


NA ELBOGAST MYALUKO
Kuelekea mchezo wa watani wa Jadi Simba na Yanga Jumapili Septemba 30, 2018, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam ambaye ni shabiki mkubwa wa klabu ya Simba Paul Makonda, amesema endapo Yanga wataifunga Simba ataanza kwenda ofisini kwa kutumia usafiri wa baiskeli.

 Makonda ametoa ujumbe huo kupitia ukurasa wake wa mtandao wa 'Instagram' akiibeza klabu ya Yanga kuwa haina uwezo wa kuifunga Simba.

"Kuna Watu wanatangaza Eti kuifunga SIMBA. Siku Simba ikifungwa na yanga nitaanza kutumia Baiskeli kwenda Ofisini. @mrisho_gambo @millardayo @hajismanara @azamtvtz"


Makonda amekuwa akishiriki katika shughuli mbalimbali za klabu ya Simba ikiwemo kwenda uwanjani kutazama mechi kadhaa za klabu hiyo.

Paul Makonda alikuwa mgeni rasmi wa mchezo wa marudiano ligi kuu ya soka Tanzania Bara kati ya Simba na Yanga msimu uliopita ambao ulipigwa April 29, 2018 na Simba kushinda bao 1-0 lililofungwa na Erasto Nyoni.

Tayari muda wa mchezo huo umeshawekwa wazi ambapo utaanza saa 11:00 jioni kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es salaam. Pia serikali imethibitisha kuwa usalama umeongezwa uwanjani hapo ikiwemo kufungwa kwa camera za kisasa zitakazobaini mashabiki watakaofanya fujo.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad