Nuh Mziwanda ndio Sababu ya Ndoa Yangu na Prezzo Kuota Mbawa- Amber Lulu

Nuh Mziwanda ndio Sababu ya Ndoa Yangu  na Prezzo Kuota Mbawa- Amber Lulu
Mwanadada Amber Lulu  amefunguka na kusema kuwa Nuh Mziwanda ndio sababu kubwa ya yeye kuachana na mpenzi wake Prezzo.

Akizungumza katika kipind cha praylist cha Times FM na kukili kuwa kuna kipind alikuwa karibu na Nuh Mziwanda na baadaye picha zake zilisambaa mitandaoni  wakiwa karibu wakijiachia kimahaba.

"Nuh ni mshikaji tu ila ndoa yangu na prezzo alimaind ile kukisiana kisiana na Nuh Mziwanda japo ni makosa tu kwakuwa mimi ni kijana na yeye yupo mbali mi nipo huku muda mwingine nahitaji vitu vingi lakini kuteleza kupo  ila nilijitahidi sana kuomba msamaha sana nikaona kama kanikazia hivi mwisho wa siku nikaona naomba msamaha sana kwaajili ya nini nikaona fresh tu kama umeamua poa wacha niishi maisha yangu" 

Amber Lulu alisema kuwa walifikia hatua nzuri japo alikuwa ajavivya pete ya uchumba ila alikuwa anafahamika kwa kina Prezzo na alikuwa na mawasiliano nao vizuri.

"Kwa sasa hivi nipo single sihitaji boyfrend wala mchumba muda ninaoupoteza kwao ni bora nifanye mambo yangu ila ikifika muda nikimtaka mtu namlipa arafu tunamalizana fresh sihitaji muda wa kusumbuana wala huyo Nuh Hata simtaki yeye mwenyewe maisha yake yanamshinda''

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad