Nyandu Tozi amebainisha hayo alipokuwa anazungumza na www.eatv.tv baada ya kuwepo minong'ono mingi kutoka kwa wadau wa hiphop wakidai wasanii wa muziki huo, wanaimba vitu vyepesi vyepesi na kuacha misingi ya hiphop yenye ambayo wanamuziki wanaimba vitu vigumu na vyenye kuelimisha.
"Trap ni muziki ambao hutumii nguvu kubwa sana kama ilivyo hiphop, kwasababu hiphop ni lazima uzame 'deep' sana ili kusudi usikosolewe katika kile unachokielezea. Mimi nafanya muziki wowote ule ambao nina amini utaweza kumfurahisha shabiki yangu kasoro taarabu tu", amesema Nyandu Tozi.
Pamoja na hayo, Nyandu Tozi ameendelea kwa kusema kuwa "kubadilika kwangu katika uwimbaji inategemeana na 'producer' atanishawishi vipi katika midundo yake atakayotengeneza, hivyo usishangae siku nikaimba singeli".
Nyandu Tozi ameonekana kubadilika katika uimbaji wake ambao watu wengi walimzoea kwa 'style' ya kuchana lakini kwa sasa ameanza ku-trap, kwenye wimbo wake mpya wa 'I don't care' aliomshirikisha Chin Bees ambao ameuachia siku tatu zilizopita tokea leo.