Polepole Atoboa Siri ya Ushindi wa Monduli na Ukonga

Polepole Atoboa Siri ya Ushindi wa Monduli na Ukonga
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa  Chama Cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole ametaja sababu za chama hicho kushinda uchaguzi jimbo la Monduli ni kuwa chama kilikuja na  mkakati  wa  kupeleka miradi ya maendeleo pamoja na kuwakopesha wananchi wanyama aina ya Mbuzi.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam Katibu huyo wa itikadi na uenezi chama hicho amesema CCM imeshinda kwa kishindo katika uchaguzi wa monduli na ukonga kwa kunadi sera za maendeleo ya miaka 5.

"Tuliwakopesha mbuzi wakulima hasa wakina mama na familia masikini tuliwakopesha mbuzi na walilipa mbuzi , kalanga akiwa upinzani lengo lilikuwa ni kuwawezesha wananchi wa monduli kiuchumi.."

Polepole pia amesema Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda  hapaswi kufanya sherehe ya kulipongeza jeshi la polisi kwa kile alichokidai waliyafumbia macho baadhi ya matukio ya uvunjaji wa amani.

"Mimi sasa hivi nasema ndugu Makonda hakutakiwa na kufanya sherehe kwa polisi, kwa sababu nimeona moja kwa moja polisi wakiwa wametulia msimamizi wa uchaguzi akifanyiwa vitendo vya kiudhalilishaji.."

Katika uchaguzi mdogo wa marudio uliofanyika septemba 16 mwaka huu CCM ilibuka kidedea katika Jimbo la Ukonga ambapo lilimsimamisha Mwita Waitara kuwa mgombea na kwa upande Monduli chama hicho kilishinda kupitia mgombea wake Julius Kalanga.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad