Profesa Jay aelezea msiba wa baba yake

Profesa Jay aelezea  msiba wa baba yake
Baba mzazi wa Mbunge wa Mikumi, Joseph Haule, 'Profesa Jay', mzee Haule, amefariki dunia leo kwenye hospitali ya St. Kizito Mikumi alikokimbizwa mapema leo baada ya hali yake kubadilika.

Profesa Jay ameongea na www.eatv.tv na kueleza kuwa mzee Haule alikuwa anasumbuliwa na presha na amekuwa akipatiwa matibabu katika hospitali ya moyo ya JKCI Muhimbili, lakini kwasasa alikuwa nyumbani Mikumi kabla ya leo hali yake kubadilika.

''Ni kweli mzee wetu amefariki leo, aliamka vizuri tu lakini baadae hali ikabadilika akapelekwa hospitali ya St. Kizito Mikumi na madaktari walijitahidi sana kuokoa uhai wake ikiwemo kuandaa 'Ambulance' kwaajili ya kumkimbiza Muhimbili lakini akafariki'', ameeleza.

Ameongeza kuwa kabla ya kifo aliomba Padri aitwe ili aweze kusali na baada ya kumaliza ndio ilikuwa inafuata hatua ya kupanda Ambulance lakini alipomaliza sala yake tu akakata roho.

Amesema taratibu zaidi za msiba watatoa taarifa baada ya kikao cha familia kwani kwasasa yupo njiani kutoka Dodoma kwenda msibani nyumbani Mikumi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad