Rage Awapa Mbinu TFF Kupata Mdhamini wa Ligi Kuu

Rage Awapa Mbinu TFF Kupata Mdhamini wa Ligi Kuu
Wakati Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) likihangaika kuzungumza na makampuni mbalimbali kuhusiana na mdhamini mkuu wa ligi, Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, amesema TFF walipaswa kufanya mazungumzo na aliyekuwa mdhamini mkuu kabla ya kufanya mabadiliko kwenye ligi.

Rage ameeleza kuwa TFF ilipaswa kukutana na Vodacom mapema ambao walikuwa wadhamini wakuu wa klabu kwa ajili ya kujadiliana na kampuni hiyo ya mawasiliano kwa ajili ya majadiliano juu ya mkataba mpya.

Kiongozi huyo aliyewahi kuingoza Simba amesema TFF walipaswa kuwajuza Vodacom mambo yapi yangeweza kubadilika ikiwemo kuongezeka kwa idadi ya timu kutoka 16 mpaka 20.

Hatua hiyo imekuja kutokana na ligi kuanza bila mdhamini mpaka sasa na baadhi ya timu zimekuwa zikilalamika juu ya gharama kadhaa ikiwemo za usafiri ambapo wengi wamesema uwepo wa mdhamini mkuu ulichangia kuleta unafuu.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad