Rais JPM Afunguka Sababu ya Kumtumbua Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje

Rais JPM Afunguka Sababu ya Kumtumbua Aliyekuwa Naibu Waziri wa Mambo ya Nje
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli ameeleza sababu ya kutengua uteuzi wa aliyekuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Suzan Kolimba ni kuwa kiongozi huyo alishindwa kuwasimamia Wakurugenzi ndani ya Wizara hiyo.


Akizungumza wakati akimuapisha Naibu Waziri mpya wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Damas Ndumbaro Rais Dkt Magufuli amesema wizara hiyo imekuwa haimridhishi kwa namna ambavyo Naibu Waziri aliyepita badala ya kuwasimamia wakurugenzi wa wizara na kusema yeye ndio alikuwa akisimamiwa na watendaji wake.

Rais Magufuli amesema "siku nyingi wizara mambo ya nje haijanifurahisha sana mambo yake mengi hayaendi vizuri, Wakurugenzi wake wengi ni dhaifu sana, wizara ile viongozi wake wanatembea sana, sio unakuwa na Naibu Waziri anayeendeshwa na Wakurugenzi badala ya kuwaagiza unachotaka wewe yani wakuongoze, ndio maana niliamua kuwatoa wote Naibu Waziri na Katibu Mkuu wake."

Awali Makamu wa Rais wa Samia Suluhu Hassani alionesha kutoridhishwa na namna ambavyo viongozi wa mambo ya nje walivyoratibu moja ya ziara ya viongozi wakubwa waliofika nchini kwa ziara ya kikazi.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad