Rais Kenyatta Asikia Kilio cha Wakenya Akubali Kupunguza Kodi ya Mafuta

Rais Kenyatta Asikia Kilio cha Wakenya  Akubali Kupunguza Kodi ya Mafuta
Rais Uhuru Kenyatta amekubali kupunguza tozo la kodi iliyopingwa na raia nchini ya 16% kwa bidhaa za mafuta nchini.

Katika hotuba kwa taifa, Rais Uhuru amependekeza kupunguza kwa nusu kodi hiyo hadi 8%

Rais Kenyatta ameeleza kwamba amesikia kilio cha Wakenya kuhusu kupanda kwa bei za bidhaa.

Awali rais Kenyatta alikataa kusaini mswada wa fedha ambao ungetoa fursa ya kusitishwa kwa tozo la kodi ya 16% kwa bidhaa za mafuta nchini.

Kumekuwa na hasira miongoni mwa raia wanaolalamika kuhusu kupanda kwa gharama ya maisha.

Miongoni mwa aliyopendekeza rais Uhuru kando na kupunguzwa kwa kodi hiyo ya mafuta kutoa 16% hadi 8% ni pamoja na kuupunguza gharama za mapokezi , burudani, mafunzo na mikutano, na usafiri katika nchi za nje.

Kadhalika amependekeza kuongezwa fedha katika idara za utekelezaji wa sheria kuweza kukusanya kipato zaidi kupitia mahakama nchini.

Ameeleza kuwa bado kuna pengo katika bajeti ya serikali na ndio sababu amependekeza hatua hizo za kufunga mkaja au kubana matumizi katika idara zote za serikali.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad