Rais Magufuli Awataka Wanawake Wajifunze Tabia Njema Toka kwa Mama Maria Nyerere

Rais Magufuli Awataka Wanawake Wajifunze Tabia Njema Toka kwa Mama Maria Nyerere
Rais Dkt. John Magufuli amewataka wanawake wote nchini wajifunze tabia njema kupitia mama Maria Nyerere, kwa kile alichokieleza kuwa hajawahi kuonyesha tabia ya tofauti tokea alivyokuwa na Hayati Mwl. Julius Nyerere hadi hii leo.

Dkt. Magufuli ametoa kauli hiyo alipokuwa anazungumza kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Mwenge uliopo wilaya ya Butiama mkoani Mara, muda mchache alipomaliza kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya makutano Natta na Mugumu yenye urefu wa kilomita 135.

"Mama Maria Nyerere wewe ni mama wa tofauti sana, ulivyokuwa na mzee wetu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere mpaka ulivyo leo tabia yako haijabadilika. Ni matumaini yangu wakina mama wengi watajifunza tabia yako maana wapo wengine wakiolewa hata na muendesha daladala anabadilika na wengine hata wakipata mwanaume mwenye kaduka hata hasalimii majirani zake...

"Wewe umekuwa mama wa taifa hili, wake wa viongozi wengi wanatakiwa wajifunze kupitia kwako. Nimeona wake za viongozi wengi na wengine huwezi hata kuwagusa. Wewe mama upo hivyo hivyo kama ulivyoletwa na Mungu hapa duniani, hongera sana mama Maria Nyerere na ni kwasababu ya malezi mazuri uliyoyapata", amesema Dkt. Magufuli.

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo alivyokuwa anaeleza umma mambo mbalimbali aliyoweza kuyafanya Hayati Baba wa Taifa, Mwl. Julius Kambarage Nyerere ambaye amezikwa katika mkoa huo.

Mbali na hilo, Rais Magufuli amesema Butiama ni sehemu ya historia ya nchi ya Tanzania na hata kama watu watapinga hilo, lakini haitoweza kubadilika jambo hilo.

Kwa upande mwingine, Rais Magufuli amesema mara baada ya kuisha mradi wa 'stigler Gorge' itabidi ubadilishwe jina kuwa 'Nyerere Gorge', ili kumpa heshima na kumuenzi Baba wa taifa ambae alitazama mbali juu ya kufanyika kwa mradi huo.

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad