Rais Magufuli Kushudia Utiaji Saini Wa Mkataba Wa Ujenzi Wa Meli Leo

Rais Magufuli Kushudia Utiaji Saini Wa Mkataba Wa Ujenzi Wa Meli Leo
Rais Dkt John Magufuli leo Septemba 03, 2018 atashuhudia utiaji saini wa mkataba wa ujenzi wa meli mpya na chelezo katika Ziwa Victoria, tukio hili linafanyika Jiji Mwanza na litarushwa moja kwa moja na TBC1, Azam Tv, ikulu.go.tz

Mikataba hiyo itahusisha ujenzi wa meli moja mpya, chelezo ya kujenga meli hiyo, ukarabati wa meli ya Mv Victoria na Butiama katika Bandari ya Mwanza Kusini jijini hapa.

Meli hiyo mpya itakuwa na uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 400 za mizigo pamoja na magari madogo 20 na itafanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba kupitia bandari ya Kemondo, Mwanza na Musoma na pia, Mwanza na bandari za nchi jirani za Kenya na Uganda.

Imeelezwa kuwa mkataba mwingine ni wa ukarabati mkubwa wa meli ya Mv Victoria yenye uwezo wa kubeba abiria 1,200 na tani 200 za mizigo, iliyokuwa ikifanya safari zake kati ya Mwanza na Bukoba kabla ya kusitisha mwaka 2014 kutokana na kuharibika kwa mitambo yake. Ukarabati huo unatarajiwa kuchukua miezi 12.

Meli nyingine itakayofanyiwa ukarabati ni MV Butiama yenye uwezo wa kubeba abiria 200 na tani 100 za mizigo, meli ambayo ilikuwa ikifanya safari zake kati ya Mwanza na Nansio Ukerewe kabla ya kuharibika mwaka 2010.

Kukamilika kwa meli hiyo kutarahisisha usafiri kwa wananchi waishio kwenye visiwa vya Ukerewe.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad