Rais Magufuli Kuzindua Flyover YA Tazara leo

Rais Magufuli Kuzindua  Barabara ya Flyover leo
Rais John Mafuguli leo anatarajiwa kuizindua rasmi barabara ya juu ya Tazara . Barabara hiyo ni daraja la kwanza la juu mjini Dar Es Salaam, inayounganisha sehemu kuu ya mji huo na maeneo makuu ya kiuchumi nchini kama uwanja mkuu wa ndege wa Julius Nyerere, Bandari na hata barabara inayoelekea Viwandani.



Kuna mchanganyiko wa hisia kufuatia kukamilika na kuanza kutumika kwa bara bara hiyo. Kwa baadhi inakuja kama ahueni kuu kutokana na msongamano mkubwa wa magari na kero la foleni zinazoshuhudiwa kila siku mjini. Barabara hiyo inajumuisha njia nne na daraja. Kwa kupunguza tatizo la msongamano na foleni inatarajiwa kuongeza muda wa watu kufanya kazi badala ya mwingi wanaopoteza wanapokwama barabarani.



Hili linatazamwa na serikali kama kufungua njia kwa wananchi kuukuza uchumi wa nchi. Kadhalika kuna wanaokosoa mradi huo kutokana na fedha zilizotumiwa kwa ujenzi huku wengine wakigusia ukubwa kwa kumithilisha na barabara nyingine za juu zilizojengwa katika nchi jirani. Ujenzi wa barabara ya juu ya Tazara unatajwa kugharimu takriban $ milioni 45.



Matayarisho yamekamilika kwa shughuli hiyo ya uzinduzi rasmi kwa mujibu wa kamishna mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda. Barabara ya juu ya Tazara ilifunguliwa tangu Septemba 15 kuruhusu waendesha magari kuijaribu kuelekea uzinduzi huu leo.



Raia katika mji wa Dar Es salaam wanatarajiwa kumiminika kuanzia hivi asubuhi katika barabara hiyo ya juu kushuhudia ufunguzi rasmi wa muundo mbinu huo nchini.Miongoni mwa walioizuru barabara hiyo wakati mradi ukielekea kukamilika ni Waziri mkuu Kassim Majaliwa. Majaaaliwa amenukuliwa akisema kwamba serikali inapanga kuzindua barabara nyingine saba kama hizo mjini Dar Es Salaam katika kukabiliana na msongamano na foleni kubwa za magari.



Ujenzi wa barabara ya juu ya Tazara ulianza Octoba 2016, kwa udhamini kamili wa serikali ya Japan.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad