Rais Magufuli: Sitatoa Chakula Cha Bure, Tufanye kazi kwa Bidii


Rais John Magufulia amewaambia wakazi wa Itilima mkoani Simiyu wachape kazi, huku akisisitiza kuwa Serikali haitatoa chakula cha bure.


Rais Magufuli ameyasema hayo jana Septemba 9, ikiwa ni siku ya pili ya ziara yake mkoani Simiyu akitokea Mara. Amewataka wananchi hao kutafuta maendeleo ya kweli hasa kwenye kilimo ambacho ndiyo shughuli kuu ya uchumi wao.


“Endeleeni kuchapa kazi, chakula cha bure hakitakuja. Hili lazima niwaambie ukweli, Serikali haina shamba,”  alisema Rais Magufuli aliposimama na kuzungumza na wakazi hao.


Rais Magufuli amewataka pia kuachana na imani za kishirikina badala yake wapeleke watoto wao shule kwa sababu Serikali inatoa elimu bure.


“Kila mwezi tunatoa Sh23.85 bilioni kwa ajili ya elimu bure. Pelekeni watoto shule,” alisema Magufuli huku akishangiliwa na wananchi hao.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad