Rais Museveni azungumzia kifo cha Askari aliyeuawa


Rais wa Uganda Yoweri Museveni jana usiku alihutubia taifa ambapo alizungumzia masuala kadhaa ambayo yameshuhudiwa nchini humo siku za hivi karibuni.

Hotuba ya rais iliangazia sana changamoto za usalama zinazoikumba nchi hiyo kwa sasa. Lakini pia alizungumzia masuala ya elimu, kilimo na miundo msingi.

Museveni alitoa hotuba yake kwa taifa saa kadhaa baada ya afisa maarufu wa cheo cha juu Muhammad Kirumira, kuuawa kwa kupigwa risasi karibu na nyumbani kwake kwenye vitongoji vya mji mkuu Kampala Jumamosi usiku.

Kirumira ambaye ni afisa aliyekuwa anakumbwa na utata aliuawa hatua chache kutoka nyumbani kwake huko Bulenga.

Mwandishi wa BBC aliye mjini Kampala anasema Museveni alizungumzia mauaji ya hivi punde ya Kirumira, aliyekuwa mbunge Ibrahim Abiriga na aliyekuwa msemaji wa polisi Felix kaweesi.

Alisema njia bora za kupambana na uhalifu zinahitaji kuanza kutumiwa kwa mfano kuwekwa alama za vidole kwenye bunduki zote.

"Kama bunduki zote zingekuwa na alama, mara unapopigwa risasi ikiondolewa na kupelekwa kwenye mashine, inaweza kutambuliwa risasi imetoka kwa bunduki namba fulani. Kama magari na pikipiki zingekuwa na namba za elektroniki sasa hivi tungekuwa tumemjua muuaji," alisema Museveni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad