Rais wa Liberia George Weah Karudi Uwanjani Kuistafisha Jezi Namba 14

Rais wa Liberia George Weah Karudi Uwanjani Kuistafisha Jezi Namba 14
Rais wa Liberia ambaye pia ni mchezaji wa zamani wa soka George Weah September 11 2018 aliingia uwanjani kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki akiwa na umri wa miaka 51 dhidi ya timu ya taifa ya Nigeria.



Weah ambaye alikuwa nahodha wa Liberia katika mchezo huo uliomalizika kwa Nigeria kupata ushindi wa magoli 2-1 yaliofungwa na Henry Onyekuru na Simeon Nwankwo, goli pekee la Liberia likifungwa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Kpah Sherman kwa penati, game hiyo ilikuwa na lengo la kuistafisha jezi namba 14 ambayo ameitendea makubwa Weah enzi zake.



Game hiyo Nigeria walitumia baadhi ya mastaa wao kama Kelechi Iheanacho na Wilfred Ndidi wanaocheza Leicester City ya England, Weah sasa jezi yake namba 14 aliyoitumia kwa muda mrefu timu ya taifa haitotumika tena kutokana na heshima hiyo Waeh ambaye anaheshima sana kwa mafanikio yake katika soka game hiyo alicheza kwa dakika 79.



Weah amerudi uwanjani September 11 katika mji mkuu wa Liberia, Monrovia ikiwa ni miaka 16 imepita toka achezee timu ya taifa ya Liberia game ya mwisho ya kimataifa, kama utakuwa unakumbuka vizuri Weah ambaye amewahi kucheza vilabu mbalimbali Ulaya kama AC Milan ya Italia, PSG na Monaco za Ufaransa ndio mchezaji pekee wa Afrika aliyewahi kushinda tuzo ya mchezaji bora wa dunia Ballon d’Or 1995.


Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad