Mshauri wa Taifa la Marekani wa masuala ya Usalama wa rais Donald Trump,John Bolton, amewaonya watawala wa Iran kwamba kutakuwa na - akitamka kwa maneno yake, jehanamu ya malipo, endapo watajaribu kuishambulia Marekani, raia wake, ama washirika wake.
Rais Trump ameyasema hayo katika mkutano wa kutoiunga mkono Iran mjini New York amesema katika kile alichokiita ''utawala wa mauaji'' wa "mullah kutoka Teheran" utakabiliana na matokeo mabaya endapo wataendelea 'kusema uongo, kudanganya, na kudanganya'.
Waziri mkuu wa New Zealand aingia katika mkutano wa UN na mwanawe mchanga
Bolton amenukuliwa akisema kuwa Marekani itakuwa kali katika kutekeleza vikwazo vya kiuchumi kwa Iran ambavyo vinaanza baada ya Marekani kujitoa katika mpango wa nyuklia wa mwaka 2015.
Alisema kuwa Umoja wa Ulaya au mtu mwingine yeyote hataruhusiwa kuwadhoofisha. Mapema waziri wa mambo ya nje nchini Marekani, Mike Pompeo, aliushutumu kwa nguvu zote Umoja wa Ulaya kwa kuanzisha utaratibu maalum wa kulipia vikwazo vya mafuta.Pompeo amedai kwamba kuendeleza mapato kwa Teheran ingeweza kuimarisha msimamo na nafasi ya Iran kama mfadhili wa serikali ya ugaidi.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa alitoa maelezo ya wazi katika hotuba yake. Antonio Guterres alikuwa muangalifu wakati wote wa hotuba yake akichelea kumlenga rais Trump kwa jina lake ingawa ujumbe wake ulikuwa dhahiri.
Ameionya dunia juu ya kutembea katika barabara ya kutajika na kutengwa kwa mara nyingine tena, na kupuuzilia mbali somo la kihostoria la karne ya ishirini,na hasa mnamo mwaka 1930 na kuhatarisha unadhifu wa kuelekea kwenye mgogoro mwingine wa kimataifa.
Baada ya hotuba za leo imefahamika wazi kuwa mkutano ulikuwa wa uwazi na ukweli kuliko wakati mwingine wowote,ingawa wakati fulani wajumbe wa mkutano huo waligawanyika katika hali isiyotarajiwa kwa muda mfupi.