Rais wa Sudan Avunja Serikali Yake

Rais wa Sudan avunja serikali yake
Rais wa Sudan Omar la Bashir jana amevunja Baraza lake la Mawaziri na kumchagua Waziri mkuu mpya ikiwa ni hatua ya kukabiliana na mzozo wa kiuchumi uliokumba nchi yake katika miezi ya hivi karibuni.

Amemteua Motazz Moussa kuwa Waziri mkuuu mpya wa nchi hiyo, ambaye anashika nafasi ya Bakri Hassan Saleh aliyechaguliwa kuongoza nafasi hiyo mwaka 2017.

Kabla ya kuteuliwa katika nafasi yake hiyo, Motazz Moussa alikuwa ni Waziri anayeshughulikia masuala ya umeme na umwagiliaji.

Uamuzi huo umekuja mara tu baada ya Rais Omar al Bashir kuitisha kikao cha dharura cha maafisa wa chama tawala katika makaazi yake katika kipindi ambacho wasiwasi wa hali ya kuuchumi imekuwa ikiongezeka kutokana na kupanda bei za vitu na vingine kutopatikana.

Hakuna nafasi nyingine za mawaziri zilizotangazwa , lakini idadi ya mawaziri katika serikali mpya itapungua mpaka 21 kutoka 31, hatua ambayo inalenga kupunguza matumizi.

Awali Naibu Mwenyekiti wa chama tawala nchini humo cha National Congress Faisal Hassan amewaambia waandishi wa habari kwamba Mawaziri wa Mambo ya Nje, ulinzi na masuala ya Rais watabaki katika nafasi zao, litakapoundwa baraza jipya la mawaziri.

Kumekuwa na upinzani tangu Januari mwaka huu, baada ya bei ya mkate kupanda maradufu, baada ya serikali kuondosha ruzuku ya chakula.

Kushuka kwa Sarafu ya Sudan kumesababisha ugumu katika kununua ngano nje ya nchi na bidhaa nyingine.

Wachambuzi wanasema kuwa uchumi wa Sudan umekuwa na matatiuzo toka Sudan ya kusini ilipojitenga na nchi hiyo mwaka 2011.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad