Ratiba ya Mechi 11 za Yanga Zamtoa Povu Haji Manara Awawashia Moto TFF

Ratiba ya Mechi 11 za Yanga Zamtoa Povu Haji Manara Awawashia Moto TFF
Ratiba ya mechi 11 za Yanga zijazo za Ligi Kuu Tanzania Baraamboyo inaonyesha Yanga watakuwa na jumla ya mechi 7 nyumbani na 4 ugenini kitendo hicho kimeonyesha kumkera Msemaji wa Timu ya Simba Haji Manara na kutoa povu zito kwenye ukrasa wake wa instagram.

Haji Manara aliandika hivi kupitia akaunti yake ya insta ''Haijawahi kutokea kokote duniani toka Ulimwengu umeumbwa!! Klabu moja kucheza mechi 12 mfululizo kwenye kituo chake..usisahau JKT,Simba,kMC na Lyon zitachezewa Taifa,,
Hoja hapa ni nn?jambo hili lingekuwa kwetu Gongowazi wangesema TFF hii ni Simba,na cc hatulalamiki tunakumbushana tu...
Hata hili la kufungiwa Meneja wetu ingekuwa wao wangehoji why Meneja wao hajafungiwa ?wakati makosa ya kina kichuya ndio aliyoyafanya Toto?
Soma bila jazba utanielewa nimemaanisha nn!!
Narudia hatulalamiki ila isije tokea kwetu halaf nisikie fyoko fyoko..Ndegelec!!!''


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad