Mkuu wa mkoa wa Dar Es Salaam Paul Makonda amefungunka mwanzo mwisho kuhusiana na namna ya kuwasaidia walemavu katika mkoa wa Dar Es Salaam yeye akiwa kama mkuu wa mkoa.
Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake Makonda ameseama ” Hapa nchini Tanzania kuna walemavu wengi mno na wanahitaji msaada wa ajira” aliongeza sheria ya mwaka 2010 namba 9 kifungu cha 31 kinamtaka mwajiri aliyeajiri wafanyakazi kuanzia 20 na kuendelea kutimiza wajibu wa kuajiri asilimia 3 ya walemavu katika ofisi yake na kuyaomba makampuni mashirika na taassisi kutoa kipaumbele kwa watu wenye ulemavu”
Mkuu wa mkoa aliongeza ” Hatuombi wapatiwe ajira kama sehemu ya upendeleo bali ni kwa kuwa wanauwezo na wamesoma lakini pia ni matakwa ya kisheria yanayotaka waajiri wote kuzingatia sheria ya ajira”
Lakini pia Makonda aliongeza kupatiwa ajira kwa walemavu kutapunguza mauaji ya walemavu mfano watu wenye ulemavu wa ngozi albino na kuyataka mashirika,makampuni na taasisi binafsi kuanza kuajiri watu wenye ulemavu wa aina yeyote na katika ofisi zinazoanzia na wafanyakazi 20 basi apatiwe ajira mtu mmoja mwenye ulemavu.
Na kutoa agizo kwa wamiliki wa makampuni,mashiriki na taasisi mbalimbali kwamba ” kuanzi sasa watu wenye ulemavu wapatiwe ajira na hadi ifikapo mwezi wa kwanza mwakani watazunguka katika makapuni taasisi na mashirika yote kuchunguza kama watu wenye ulemavu wamepatiwa ajira tayari”