RC Makonda atangaza kuvuna milioni 346


Baada ya kuendesha kampeni ya usafi kwa mwezi mmoja, mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda ametoa taarifa ya kampeni hiyo, ambapo ameeleza imezalisha kiasi cha shilingi milioni 346.

Makonda amebainisha hilo leo kwenye mkutano uliofanyika jijini Dar es salaam na kuhusisha wadau wa afya na mazingira.

''Katika kampeni hii zaidi ya watu 1,0000 wamekamatwa kati yao watu 4443 waliachiwa huru, 376 walipata dhamana na watu 6 bado wapo mahakamani huku takribani watu 6577 wakilipa faini iliyofikia shilingi milioni 346.6.

Makonda ameongeza kuwa kutokana na mkoa kutokuwa na fedha ya kuwalipa mgambo wanaosimamia zoezi hilo hivyo nusu ya fedha hizo zimetumika kama malipo kwa mgambo wanaosimamia usafi.

Aidha mkuu huyo wa mkoa amesisitiza kuwa yeye kwa pamoja na wakuu wa wilaya wamelaani kitendo cha mgambo kumpiga raia katika eneo la Bunju na wamefuatilia na hadi sasa watuhumiwa wapo katika gereza la Segerea.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad