Baada ya taarifa kusambaa kuhusiana na kifo cha rapper Mac Miller 26′ aliyefariki September 7,2018 na kifo chake kuhusishwa na matumizi ya dawa za kulevya “Over Dose” akiwa nyumbani kwake San Fernando Valley Marekani mamlaka ya usalama wametoa ripoti.
Polisi wametoa ripoti kuhusiana na taarifa za kifo hicho na kusema kuwa kutokana na uchunguzi walioufanya katika nyumba ya Marehemu Mac Miller hawajakuta aina yoyote ya dawa za kulevya zaidi ya kukuta kiasi kidogo cha unga mweupe na haileti maana mtu kufariki nyumbani kwake kutokana na matumizi ya dawa za kulevya halafu nyumba ibaki bila kithibitisho chochote.
Mac Miller aliwahi kuwa mapenzini na mwanadada Ariana Grande kwa miaka miwili na kuachana mwanzoni mwa mwaka huu na kudaiwa kuwa marehemu alianza matumizi ya dawa za kulevya baada ya kuachana na Ariana Grande. Mwili wa Mac Miller umepelekwa hospitalini kwa uchunguzi zaidi.
Ripoti za Polisi Kuhusu Kifo cha Rapper Mac Miller
0
September 08, 2018
Tags