www.eatv.tv ilianza kwa kumtafuta kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara Agustino Senga, ambaye amesema amefuatilia lakini taarifa alizopata ni kwamba mbunge huyo hayupo Manyara bali yupo wilayani Monduli kwenye uchaguzi.
''Katika eneo langu nimefuatilia kwa watendaji wangu hakuna tukio hilo lakini nimeelezwa mbunge huyo yupo kwenye mambo ya uchaguzi huko Monduli labda uwasiliane na kamanda wa Arusha'', amesema.
Katika kutaka kujua ukweli wa taarifa hiyo www.eatv.tv ikamtafuta kamanda wa polisi mkoa wa Arusha (SACP) Ramadhani Ng’anzi, ambaye naye amesema hana taarifa juu ya tukio hilo huku akieleza mpaka sasa hali ni shwari katika uchaguzi wa Monduli.
''Tukio hilo sijalipata huku kwangu maana uchaguzi unaendelea vizuri watu ni wengi, usalama ni wa kutosha labda kama itabainika hivyo nitatoa taarifa lakini kwasasa sina taarifa hiyo'', amesema kamanda Ng'azi.
Taarifa inayosambaa mtandaoni inaeleza kuwa gari la mbunge huyo limeshambuliwa kwa tairi zake kupigwa risasi. Tutaendelea kukufahamisha undani wa tukio hili kadri tunavyopata taaarifa.