Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds FM, Ruge Mutahaba, na Msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Nikki wa Pili wamemmwagia sifa za kutosha Muandaaji wa shindano la Miss Tanzania 2018, Basilla Mwanukuzi.
Basilla Mwanukuzi.
Ruge kwenye barua yake ya pongezi amesema Bi. Basilla amerudisha heshima ya shindano hilo ambalo lilikuwa linaonekana kupoteza sifa yake kwa miaka ya hivi karibuni.
“Basila Hongera sana mdogo wangu, kikubwa ulichofanikisha kufanya ni kuanza kurudisha imani kwa waliopoteza imani na hiyo brand. Sio siri, itakuchukua mwaka mmoja, miwili hata mitatu kufika kwenye level ya kupata the same integrity na value iliyokuwa imepotea. Kurudisha imani za wadhamini, wahisani na mwisho sisi wananchi tutarudi labda kwa ukubwa kuliko ilivyokuwa. Umefanya makosa mengi sana kwenye hii hatua ila ni sehemu ya ukuaji because najua hakuna mtoto anajaribu kutembea bila kuangukaanguka. Kama Clouds Media Group tupo na wewe na mawakala wote kwa pamoja mmewezesha jambo hili kurudi kupata heshima yake. Kubwa kuliko yote ili kujenga heshima inayodumu ungalizi wa washindi uendelee kwa muda mrefu kupata role models wengi kwa taifa letu. Mungu awabariki sana.“ameeleza Ruge.
Kwa upande mwingine, Nikki wa Pili naye amemmwagia sifa muandaaji huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuandika
“Nimpongeze mwandaaji wa miss tanzania @basillamwanukuzi kwanza kwakuwa ni mwanamke(yes) pili kuona fursa katika passion yake ya urembo, tatu kuirudisha misstanzania iliyo kuwa imepotea, nne kwa kuanza na kidogo lengo si zawadi lengo kujenga brand ya misstanzania na warembo pia……..Nachosema songa mbele ifanye kuwa taasisi itengeneza pesa na ajira mwaka mzima…….warembo wa 5 waliopata ajira nao wata tengeneza ajira kwa wapiga picha, wabunifu, na watu wa branding, media zimepata content, biashara zimetangazwa, watu wamepata burudani na fursa kibao umezifungua ni kwa vijana kufikiria kuziendeleza kutokea jana kwenda mbele..#wenye wingi wa lawama wana uchache wa kuona fursa.“.
Jana usiku kulikuwa na shindano la Miss Tanzania 2018 ambapo mrembo, Queen Elizabeth aliibuka kidedea kwa kuwamwaga wenzake 19.