Katika uvumbuzi unaotumia teknolojia ya kisasa, vijana wawili nchini Rwanda wametengeneza kifaa cha kielectroniki kinachoweza kusimamisha gari mara moja baada ya kutambua kwamba dereva amekunywa kiwango fulani cha pombe.
Kifaa kinachotambua dereva mlevi na kusimamisha gari chabuniwa Rwanda
Kwa mujibu wa BBC, vijana hao wanasema kifaa hicho kitasaidia kupunguza ajali za barabarani ambazo husababishwa na ulevi wa kupindukia.
“Tuseme kwamba nawasha gari nikiwa sijakunywa pombe yoyote , hiki kifaa hapa kinaonyesha kwamba hali ni ya kawaid, lakini ngoja ninywe pombe hapa kidogo”, Fiston Rutikanga akinionyesha jinsi kifaa alichotengeneza kinavyofanya kazi.
Kifaa kinachotambua dereva mlevi na kusimamisha gari chabuniwa Rwanda
“Halafu nikipumua kwa kuelekeza kwenye kifaa hiki, screen hapa inaonyesha asilimia ya kiwango cha pombe uliokunywa na ikifika kile kiwango cha juu tulichopanga,gari linajisimamisha, lakini kwanza dereva anapata ujumbe mfupi kwa simu yake.” Anaeleza.
Ni kifaa cha electroniki kinachonusa harufu na kutambua kiwango cha ulevi kama dereva amekunywa pombe.
Ni mradi uliotengenezwa na Fiston Rutikanga akishirikiana na mwenzie Izere Honore vijana wanaosomea uhandisi katika chuo cha ufundi cha Rwanda kama njia ya kusaidia kupunguza ajali za barabarani
“Ikishaandikwa kwamba unakatazwa kwendeshaka kamwe huwezi kuwasha gari tena hata ufanye nini, gari haliwezi kuwaka. Ni mpaka utafuta dereva mwingine ambaye hana harufu ya pombe na kuzima mfumo mzima wa kifaa hiki na kuwasha upya halafu gari pia liweze kwenda tena”.
Kifaa kinachotambua dereva mlevi na kusimamisha gari chabuniwa Rwanda
Kifaa hicho husaidiwa na nyaya zilizosimikwa kutoka ndani ya injini ya gari. Lakini inakuwaje ikiwa ndani ya gari siyo dereva aliyelewa au mtu aliyekaa karibu naye?
“Kifaa hiki kinanusa harufu ya dereva peke yake .Tulivyokitengeneza tuliweka kama mipaka ya unusaji. Unusaji unaishia eneo la dereva peke yake abiria wa pembeni au abiria wanaokaa sehemu ya nyuma ya dereva hata wawe wamelewa chakari, harufu yao haiwezi kusababisha gari kusimama kwa sababu kifaa hiki kinahisi na kutambua harufu ya eneo tu la dereva.”
Ameongeza kwamba gari haliwezi kusababisha ajali barabarani kwani programu hii inampa dereva muda wa kuegesha gari pembeni kabla kuzima.
Kifaa kinachotambua dereva mlevi na kusimamisha gari chabuniwa Rwanda
Kifaa kinachotambua dereva mlevi na kusimamisha gari chabuniwa Rwanda
Uvumbuzi wa vijana hawa wanasema wameuweka katika mradi walioita SAFETY DRIVING WITH SECURITY ukichanganya progamu ya gari kujisimamisha kwa kuhisi tu harufu ya pombe na programu nyingine ya kudhibiti mwendo kasi , ama (speed governor).
Mradi huo wanasema umeshatambuliwa na mamlaka ya maendeleo ya Rwanda, mamlaka ya ubora wa bidhaa na polisi ikiwa imebaki kazi ya kunyoosha kifaa hicho kiwandani kabla ya kukiweka sokoni
Rutikanga Azungumzia kifaa Alichovumbua ‘ Gari linajisimamisha lenyewe Ukiwa Umelewa, Haliwaki Hata Ufanye Nini
0
September 27, 2018
Tags