Samatta Aonyesha Nia Yake ya Kumiliki Ndege Binafsi

Samatta Aonyesha Nia Yake ya Kumiliki Ndege Binafsi
Mchezaji wa kimataifa wa mpira wa miguu Mbwana Ally Samatta wengine hupenda kumwita "SAMA GOAL" ambaye anaichezea timu ya Genk ya ubelgiji kama  mshambuliaji na pia anaichezea Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars, ametangaza nia na ndoto ya kupigania kumilika ndege binafsi, hiyo ni baada ya kupiga picha kwenye ndege na kuahidi kuanza vita dhidi ya kutimiza lengo lake hilo.

Kama ulikuwa Hujui nikujuze tu,  Mbwana Ally Samatta amezaliwaTarehe 7 mwenzi wa 1 mwaka 1992, alianza kucheza mpira katika klabu ya African Lyon mwaka 2008 hadi 2010 alipohamia katika klabu ya Simba  na 2011 alihamia katika klabu ya Congo ambayo ni TP Mazembe aliweza kufunga magoli 60 pia katika timu ya taifa ya Taifa stars amefunga magoli 9, Samatta anajulikana sana katika mji wa Lubumbashi kwa kuwa alifunga magoli sita katika mashindano ya ligi ya mabingwa Africa na kuiwezesha Mazembe kutwaa kombe hilo.

Samata amekuwa mfungaji bora katika ligi ya mabingwa Africa na Tarehe 7 mwenzi wa 1 mwaka 2016 Samata ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa Africa kwa wachezaji wa ndani, pia ni mtanzania wa kwanza kutwaa taji hilo la ligi ya mabingwa Africa pamoja na Thomas Ulimwengu, mwaka huo huo alijiunga na timu ya Genk ya huko ubeligiji 

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad