Alfajiri ya leo (Jumanne) Kepteni wa Taifa Stars, Mbwana Samatta ametua nchini akitokea Ubelgiji kwa ajili ya kujiunga na kambi ya timu ya taifa.
Samatta ametua akiwa pamoja na mchezaji mwenzake Thomas Ulimwengu anayecheza Al Hilal ya Sudan.
Taifa Stars inajiandaa na mchezo wa kutafuta tiketi ya kufuzu Afcon dhidi ya Uganda utakayochezwa Septemba 8, 2018 huko Uganda.
Wachezaji wengine wa Stars wanaocheza soka nje ya nchi ambao wamewasili kwenye kambi ya timu ya taifa ni Rashid Mandawa na Ramadhani Kessy.