Kampuni ya Samsung imetangaa ujio wa simu mpya za Galaxy A7 (2018) ambapo inakuwa toleo lao la simu ya kwanza yenye Kamera tatu kwa nyuma.
Ujio wa Galaxy A7 (2018) inaelezwa kuwa huenda ukadhoofisha manunuzi ya matoleo mapya ya simu za iPhone XS, XS Max na iPhone XR, hii ni kutokana na bei yake kuwa ndogo na yenyewe kuwa na sifa nyingi sawa na matoleo hayo.
Simu hiyo, Kamera tatu za nyuma zina ukubwa wa Megapixel 24, 8 na 5 huku zikisaidiwa na LED flash (LCD) . Sifa nyingine ni kwamba ina kioo (screen) ya ukubwa wa inchi 6 kilichotengenezwa na teknolojia ya Super AMOLED Display chenye resolution ya 1080 x 2220 .
Simu hii pia inakuja na processor yenye Octa-Core 2.2 GH’s inayosaidiwa na RAM ya GB 4 na GB6 huku ukubwa wa ndani ukianzia GB 64 na GB 128.
Kupitia mtandao wa Samsung wamesema simu hii itauzwa Euro 350 sawa na Tsh 942,000 bila makato ya kodi. Na inatarajiwa kuzinduliwa Oktaoba 11 mwaka huu.
Samsung Watangaza Balaa Lingine, Hili ni Tishio kwa Matoleo Mapya ya iPhone X’s
0
September 26, 2018
Tags