Serikali Kupitia Kamati ya Ulinzi Dar Yafanya Ziara Feri Kigamboni YAgundua Changamoto Hizi Kwenye Vivuko

Serikali Kupitia Kamati ya Ulinzi Dar Yafanya Ziara Feri Kigamboni YAgundua Changamoto Hizi Kwenye Vivuko
Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Kigamboni jijini Dar es salaam imefanya ziara ya kutembelea vivuko vya Feri na kubaini changamoto tatu zinazovikabili vivuko hivyo na kutishia usalama wa watumiaji.


Changamoto hizo ni kutokuwepo kwa namba za dharura ndani ya kivuko na eneo la kusubiri kivuko, kutofanya kazi kwa runinga zilizopo kwa ajili ya kutoa elimu ya namna ya matumizi ya vivuko na kamera maalumu za kurekodi matukio ya kinachoendelea ndani ya chombo hicho cha usafiri.

Kamati hiyo imefanya ziara leo Jumatano Septemba 26, 2018 ikiongozwa na mwenyekiti wake, Sarah Msafiri ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kigamboni.

 Akizungumza baada ya kufanya ziara hiyo DC Sarah Msafiri, amesema hajaridhishwa na namna vivuko hivyo vinavyotoa huduma hasa cha MV Magogoni kinachobeba watu 2000 na magari 60.

“Vifaa vya uokozi vipo lakini hakuna matangazo wala elimu inayotolewa ya namna ya kuvitumia vitendea kazi hivyo pindi linapotokea tatizo, hii ishu ya kuzama kwa MV Nyerere imetokea wakati ratiba yangu ya kutembelea vivuko hivi ilikuwapo kama kawaida”, amesema Msafiri.

Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni siku mbili baada ya kituo cha EATV kutoa taarifa juu ya kuwepo kwa boti ndogo zinazobeba abiria kinyume na utaratibu kutoka fukwe ya Kigamboni kuja fukwe ya Feri ambapo DC Msafiri amepiga marufuku boti hizo kufanya biashara hiyo na amemuagiza mkuu wa Polisi wa Kigamboni kuzikamata boti hizo kuanzia leo na kuchukuliwa hatua.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad