Serikali ya Uingereza Kutoa Nguvu Kuandaa Kombe la Dunia

Serikali ya Uingereza Kutoa Nguvu Kuandaa Kombe la Dunia
Waziri mkuu wa Uingereza Theresa May, amesema endapo chama cha soka nchini humo (FA), kitaamua kuomba kuandaa kombe la dunia 2030 watatoa nguvu yote kuhakikisha wanafanikiwa hata kwa kushirikiana na Jamhuri ya Ireland.


May ametoa kauli hiyo wakati akihutubia kwenye mkutano wa mwaka wa chama chake cha 'Conservative' uliofanyika jana mjini Birmingham Uingereza.

''Timu yetu imefanya vizuri sana kwenye fainali za kombe la dunia mwaka huu, tunatamani zifanyike kwenye ardhi yetu baada ya miaka mingi kupita, kama FA wataomba sisi kama serikali tutahakikisha tunakuwa nao pamoja mpaka tufanikishe hilo'', aalisema.

England iliandaa michuano ya kombe la dunia mwaka 1960, ambapo ilianza Julai 11 hadi 30. England waliibuka mabingwa kwa kuwafunga Ujerumani kwa mabao 4 - 2 Ujerumani Magharibi.

Taifa hilo pia lilikuwa miongoni mwa mataifa makubwa yaliyokuwa yameomba kuandaa fainali za mwaka 2018 kabla ya kushindwa na Urusi. Mara ya mwisho England kuandaa michuano mikubwa ilikuwa ni mwaka 1996 ambapo iliandaa Euro.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad