Serikali yaagiza kukamatwa mmiliki wa Lori lililoua watu 15


Serikali imeagiza kukamatwa na kuwekwa mahabusu mmiliki wa lori lenye namba za usajili T 334 DJN mali ya kampuni ya Azania Group ambalo lilifeli breki likiwa kwenye mteremko mkali wa Iwalanje, eneo la Igawilo Jijini Mbeya kabla ya kuyagonga magari mengine manne na kusababisha vifo vya watu 15 na kujeruhi wengine 13. 

Naibu Mawaziri wawili ambao ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Hamad Masauni na Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Elias Kwandikwa wamewasili kwa pamoja Jijini Mbeya na kutembelea eneo la ajali kisha kukagua barabara ya Tukuyu - Mbeya hususan katika eneo lenye mteremko na kona kali za Iwalanje. 

Kwa upande wake Kwandikwa amesema barabara hiyo ya Tanzania - Malawi ni miongoni mwa barabara chache nchini ambazo ziko kwenye ubora hivyo ajali hiyo haitokani na matatizo ya barabara na kudai kuwa upo umuhimu wa kuchukua hatua za kupunguza makosa ya ubinadamu barabarani.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad