Serikali Yapiga Marufuku Kuhusu Sukari

Serikali yapiga marufuku kuhusu sukari
Serikali kupitia Wizara ya Viwanda na Biashara imepiga marufuku wafanyabiashara wa sukari nchini kupandisha bei ya bidhaa hiyo kiholela na kutotumia uhuru walionao kuwaumiza wananchi.


Agizo hilo limetolewa leo Bungeni na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ,Stella Manyanya, wakati akijibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mbunge wa Mbulu Mjini Zacharia Paul juu ya uzalishaji wa sukari na bei zake.

Mh. Zacharia alihoji kwanini serikali isizalishe sukari ya kutosha ili kuepuka mfumuko wa bei inayotokea kuanzia mwezi wa 3 kila mwaka, ndipo Naibu Waziri akamjibu juu ya viwanda nchini kuwa na uwezo wa kutosha wa kuzalisha sukari wawekezaji wamekuwa wakitumia vibaya uhuru wa kupanga bei.

''Pamoja na kwamba wawekezaji au wazalishaji wa sukari ni wafanya biashara binafsi na serikali tumekuwa hatuwaingilii sana katika upangaji wa bei lakini natoa rai kwao iwe mwiko kupandisha bei ya sukari kiholela'', amesema Mh. Manyanya.

Awali Waziri wa Viwanda na Biashara Charles Mwijage, ameeleza kuwa vyombo vya dola vinaendelea na uchunguzi juu ya wafanyabiashara wanaoingiza nchini sukari ya magendo na kuharibu biashara ya viwanda vya ndani.

''Kwenye suala la wawekezaji kuingiza sukari za magendo kutoka nje ya nchi kuna jinai ndani yake na vyombo vya dola vinafuatilia na wako makini naomba nisiendelee sana ila anayehusika atakiona cha moto'', amesema Mwijage leo Bungeni.
Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad